
Dereva wa daladala Maarifa Matala (45), mkazi wa Kimara Suka mkoani Dar es Salaam anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake, Sharifa Nyamaishwa (31) Kondakta wa daladala, mkazi wa Kimara Suka, kwa kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake na kumuua kutokana na wivu wa kimapenzi.
.
Hata hivyo, Jeshi hilo limebainisha kuwa uchunguzi wa shauri hilo unakamilishwa na Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo.
