Back to top

Dereva wa Basi la Presidar anaswa na polisi.

11 July 2020
Share

Jeshi la polisi mkoani Iringa limefanikiwa kumkamata dereva wa basi la kampuni ya Presidar lililosababisha ajali na iliyochukua maisha ya watu kumi na majeruhi kadhaa siku chache zilizopita.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire ametoa taarifa ya kukamatwa kwa dereva huyo anayedaiwa kuwa baada ya ajali alitoroka na kwenda kujificha kwa baba yake mdogo wilayani Mbarali.