Back to top

DJUMA SHABANI AFUNGUKA KWA WAKONGO ANACHOFANYIWA YANGA

05 July 2023
Share

Mchezaji wa Yanga Djuma Shabani, ambaye ana mkataba na timu hiyo mpaka 2024, amesema ana furaha sana kucheza soka la Tanzania kwa sababu viongozi wa soka wanajua kuwahudumia vyema wachezaji.

Djuma Shabani amezungumza na mwanahabari wa umoja wa wachezaji wa Congo Ufs, Olivier Sefu na kumwambia wachezaji wa Kitanzania hawana matamanio tena ya kuja kucheza Congo DR kama enzi za Mbwana Ally Sammata

Amesema ligi ya Congo- DR inatia hofu kwa sababu inakosa wasimamizi makini na uratibu mzuri wa ligi huku wachezaji wakipitia kipindi kigumu.Na kusema kama hawatabadilika basi wasiwe na matumaini yoyote. 

Amesema Tanzania ligi haisimami hovyo kama Congo ambako amesema viongozi wanavipaumbele vyao na wala hawachukuliwi hatua huku akipigilia msumari kuwa Tanzania kila klabu inanufaika na haki za matangazo ya televisheni na akiisifu ligi ya Tanzania kuwa na hadhi ya juu kwa kushika nafasi ya 5.