Back to top

DK. MOLLEL: TUSHIRIKIANE HAMASA BIMA YA AFYA KWA WOTE.

02 February 2024
Share

Serikali imetoa wito kwa Watanzania, Viongozi wa kisiasa, kidini na kimila kuungana na Serikali katika kuhamasisha umma kujiunga na Bima ya Afya kwa wote pale mchakato utakapoanza rasmi.
 
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mhe. Tarimba Gulam Abbas Mbunge wa Jimbo la Kinondoni.

Dkt. Mollel amesema kuwa nchini kuna watoto Milioni 31, milioni 1.5 wako kwenye mfumo wa Bima ya afya ya sasa, na milioni 30.7 wako kwenye mifumo ya bima za afya nyingine zilizopo nchini.

“Niwahakikishie wananchi kuwa ujio wa bima ya afya kwa wote utakuwa suluhisho la changamoto ya matibabu kwa wananchi wote bila kujali hali ya kiuchumi na kikwazo cha fedha, hivyo naomba mchakato utakapoanza wananchi mjitokeze kujiunga na skimu za zitakazobainishwa ambazo zitakua kwa rika zote”. Ameeleza Dkt. Mollel.