
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafisa Wakuu wa Biashara (STO) wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) ,Dkt. Hashil Abdallah ,amezisisitiza nchi wananchama kuandaa sera zitakazoweza kuondoa vikwazo, kukuza ushirikishwaji na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi hizo.
Dkt. Abdallah ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa 16 wa Kamati ya Maafisa Wakuu wa Biashara wa AfCFTA, unaofanyika Durban, Afrika Kusini, ukiongozwa na Tanzania, ambayo ni Mwenyekiti wa AfCFTA kwa mwaka huu 2024.
Akifungua Mkutano huo, Dkt. Abdallah amezitaka nchi wananchama wa Mkataba huo kuhakikisha kuwa faida za AfCFTA zinafika pembe zote za Bara la Afrika.
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (Usimamizi na Uchumi) Bw. Elijah Mwandumbya, amesema Mkutano huo unalenga kutatua masuala ya kikodi, ili kurahisisha biashara katika Bara la Afrika.
