Back to top

Dk.Gwajima: Walioiba dawa Hospitali ya Ukerewe wachukuliwe hatua.

14 January 2021
Share

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima, ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu na maadili watumishi sita wa Hospitali Ya Wilaya Ya Ukerewe mkoani Mwanza ya Nansio waliohusika na wizi wa dawa zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200.
.
Dk. Gwajima ametoa agizo hilo wakati alipofanya ukaguzi wa huduma za afya zinazotolewa na hospitali hiyo, inayotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa hospitali ya mkoa baada ya kuelezwa kwamba watumishi hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza na kutozwa faini ya shilingi milioni 100 baada ya kukiri makosa yao.
.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Cornel Magembe amedai iwapo hatua za kuwasimamisha kazi watumishi hao, akiwemo mganga mfawidhi wa hospitali Hiyo Dk. Revocatus  Cleophace na Mfamasia Exavery Kamenye hazitachukuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, atalifikisha suala hilo kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli.