Back to top

Dk.Mpango aitaka TRA kukusanya kodi kwa kuzingatia sheria za nchi.

04 April 2021
Share

Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewataka Watumishi wote wa Umma na Watanzania kufanya kazi kwa Bidii, Uadilifu na weledi pamoja na kumtanguliza Mwenyezi Mungu.

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango ameyasema hayo alipokuwa katika Ibada ya Misa Takatifu ya kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.

Aidha Makamu wa Rais Mhe. Dkt.Mpango ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kukusanya kodi kwa kuzingatia sheria za Nchi na kuwaacha Wafanya Biashara wafanye Biashara zao kwa Haki na kutowanyanyasa kwenye Biashara zao ili kuleta kodi kwa ajili ya kuweza kuwahudumia Watanzania.

Katika Ibada hiyo Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango pia amewasilisha salam za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwaomba Waumini hao na Watanzania kwa ujumla waendelee kumuombea Rais Samia na kuiombea Nchi ili iweze kuneemeka zaidi ya hapa ambapo Rais Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ametufikisha.

Katika salamu hizo Mhe.Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania anawatakia Watanzania wote heri ya Sikukuu ya Pasaka na kuendelea kufanya kazi ili kuweza kuijenga Nchi yetu ya Tanzania.