Back to top

Dk.Mpango alishukuru shirika la Teresia mtoto wa Yesu kutunza yatima

05 April 2021
Share

Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Dk. Philip Mpango amelishukuru Shirika la Teresia wa Mtoto Yesu, lenye Makao Makuu yake nchini India kwa kazi nzuri wanayoifanya kuisaidia Tanzania katika kazi ya kuwatunza Watoto yatima, wazee  na watu wenye mahitaji maalum.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo katika Kituo cha Kuwatunza Watoto Yatima, Wazee  na Watu wenye Mahitaji Maalum cha Huruma Missionary Sisters of Charity kiliopo Hombolo Jijini Dodoma.

Makamu wa Rais amesema ataihimiza Wizaya ya Afya na Maendeleo ya Jamii, kitengo cha Ustawi wa Jamii wafike katika Kituo hicho chenye watu 90 wafanye  kazi ya kutoa huduma zaidi.