Back to top

DKT KIJAZI ATAKA MAAFISA HABARI WA SERIKALI KUTOA ELIMU YA SENSA.

12 May 2022
Share

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Allan Kijazi amewataka maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa sensa ya Makazi na watu imayotarajia kufanyika Agosti 2022.
 
Dkt.Kijazi alisema hayo mkoani Tanga tarehe 12 Mei 2022 wakati akiwasilisha mada kuhusiana na Sensa ya Makazi kwenye kikao cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kinachoendelea mkoani Tanga.
 
"Ninyi Maafisa Habari mnatakiwa kuelimisha wananchi umuhimu wa taarifa za majengo na ni kwanini ifanyike wakati huu"Amesema Dkt. Kijazi.
 
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ni vizuri Maafisa Habari wakashiriki vyema katika zoezi hilo kwa kutoa elimu sambamba na kubainisha changamoto na kutoa mrejesho hata kabla ya kuanza kwa sensa ya makazi.

DKt.Kijazi alisema, takwimu zitakazopatikana wakati wa zoezi la sensa ya watu na makazi zitaisadia serikali kupanga na kutekeleza mipango yake itakayoleta mabadiliko katika maendeleo ya kiuchumi.