Back to top

Dkt. Kikwete ateuliwa kuwa Mwenyekiti Jopo la Wazee SADC.

02 March 2022
Share

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Jakaya Kikwete ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Jopo la Wazee wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) litakalokuwa linashughulikia migogoro katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
.
Dkt. Kikwete anachukua nafasi hiyo baada ya Mwenyekiti wa Jopo hilo ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Botswana Dkt. Mokgweetsi Eric Keabetswe kumaliza muda wake.