Mwenyekiti mtendaji wa Makampuni ya IPP Dokta Reginald Mengi ametaka balozi wa ufaransa hapa nchni Bwana Frederick Clavier kujenga ushirikiano wa wajasiriamali wa wadogo kati ya Ufaransa na Tanzania hususani katika kuongeza thamani bidhaa za Tanzania ili ziweze kuuzwa nchni Ufaransa katika mfumo utakaowezesha pande zote mbili kunufaika.
Akizungumza na balozi Frederick Clavier na ujumbe wake walipomtembelea ofisi kwake 26 March 2018, Dokta mengi amesema tunapozungumza swala ushirikiano katika uwekezaji tunaangalia uwekezaji mkubwa na kwamba hatuwezi kukuza uchumi bila ya kushirikisha wajasiliamali wadogo na wakati kwa kuwa wana nafasi ya kukua.
Katika mkutano huo balozi wa Ufaransa hapa nchni Bwana. Frederick Clavier amesema serikali ya Ufaransa iko huru kufanya kazi na Tanzania na inampango mkakati wa muda mrefu kwa kuwa kuna fursa nyingi katika miundo mbinu, magezu ya viwanda na kilimo na kadhalika na katika kusaidia azma ya Tanzania ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, ambapo imeongeza fedha za maendeleo kwa Tanzania kutoka Euro Milioni 50 hadi Euro Milioni 100.
Aidha Dokta Reginald Mengi amemweleza Balozi Frederick Clavier kuwa muda sahihi wa kuwekeza hapa nchini Tanzania ni sasa sababu kuna sera sahihi za uwekezazaji na Rais sahihi, huku Balozi wa Clavier ameyaomba makampuni ya IPP kwa kushirikiana na tasisi ya sekta binafsi kushirikiana na ujumbe wa wafanyabiashara wa Ufaransa wanaotarajiwa kuingia nchni mwezi ujao.