Back to top

DKT.BITEK0 AIAGIZA TANESCO KUJENGA LAINI MPYA YA UMEME USHIROMBO

07 June 2024
Share

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt Doto Biteko, ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kujenga laini mpya ya Umeme kutoka Nyakanazi-Ushirombo na Kahama Bongwe hadi Bukombe ili kuhakikisha hali ya upatikanaji wa umeme katika  Wilaya ya Bukombe inaimarika.

Dkt.Biteko ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Bukombe, Mkoa wa Geita ambapo amesema kuwa sambamba na ujenzi wa laini hizo za umeme, kutajengwa kituo cha kupoza Umeme Bukombe ili kuhakikisha wananchi wakiwemo wa Ushirombo wilayani Bukombe wananufaika na umeme wa uhakika.

Kuhusu uwepo wa umeme wa kutosha nchini, Dkt. Biteko amesema Serikali imefanya kazi kubwa ya  kuhakikisha wanaondoa mgao wa umeme  kwa kuongeza vyanzo mbalimbali vya uzalishaji umeme na hivyo  kuondoa tatizo la kukatika mara kwa mara kwa nishati hiyo.