Back to top

DKT.JINGU AITAKA MSD KUWAJALI WATEJA

15 December 2023
Share

Bohari ya Dawa (MSD), imetakiwa kuwajali wateja na kuwashirikisha katika suala zima la kuwapa huduma za mnyororo wa ugavi wa bidhaa za Afya nchini.
.
Maelekezo hayo yametolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu, wakati  akifungua kikao cha 22 cha Baraza la Wafanyakazi wa MSD, kilichofanyika Mkoani Morogoro ambapo amesisitiza kuwa, kujali wateja ni msingi wa kuwahudumia kulingana na mahitaji yao.
.
Aidha, Dkt. Jingu amesisitiza umuhimu wa MSD kujiendesha kibiashara na kuwa wabunifu ili kuweza kuleta ufanisi na tija katika jamii.
.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Mavere Tukai amesema kuwa MSD ni miongoni mwa Taasisi za kimkakati na imeanza kujiendesha kibiashara.