Back to top

Dkt.Jingu apongeza zoezi la Anwani za Makazi, Mbeya

17 May 2022
Share

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. John Jingu amepongeza maendeleo ya utekelezaji wa zoezi la Anwani za Makazi Jijini Mbeya wakati alipokutana na Kamati ya utekelezaji wa zoezi hilo mkoani humo.
.
Dkt.Jingu Ametoa pongezi hizo alipotembelea na kukagua utekelezaji wa anwani za makazi mkoani humo.
.
Aidha alikagua shughuli za uchakataji wa vibao vya nyumba pamoja na nguzo za barabara na mbawa zake vinavyotengenezwa katika karakana ya Allyrich iliyopo eneo la Soweto alielekeza kuongeza kasi ya utengenezaji kwa kushirikiana na Watendaji wa Kata ili kuhakikisha zoezi linakamilika kwa wakati.
.
Dkt Jingu aliwashauri wakandarasi hao kushirikiana na mhandisi ili kuweza kupunguza gharama za nguzo na zoezi la kazi hiyo kukamilika kwa wakati.