Back to top

DKT.KIJAZI ATAKA WATAALAMU WA UTHAMINI WAJITATHMINI KATIKA UTENDAJI.

30 June 2022
Share

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Allan Kijazi amewataka wataalamu wa uthamini kujitathmini katika kazi wanazozifanya ili kuepuka kufanya kazi kwa matakwa ya wale wanaowafanyia kazi.

Amesema zipo tafiti mbalimbali zilizofanyika zikionesha asilimia kubwa ya kazi zinazofanywa na wataalamu wa uthamini zina ushawishi wa watu wanaozihitaji jambo alilolieleza kuwa halileti picha nzuri.

"Tafiti zinaonesha kazi nyingi mnazozifanya asilimia kubwa zinakuwa 'Influenced' na matakwa ya wale wanazohitaji hivyo haileti picha nzuri kama watendaji wa serikali na wale walioaminiwa kukabidhiwa kazi"Amesema Dkt.Kijazi

Akizungumza wakati wa kufungua kikao kazi cha siku mbili cha wataalamu wa uthamini kinachoendelea Jijini Dodoma leo 30 Juni 2022, Dkt Kijazi amewaambia wataalamu hao kuwa, wakati wakiendelea na kikao chao ni vyema wakajitathmini na kujiuliza ni nini kifanyike kuzuia hali hiyo isiendeleeea kwa kuwa inasabisha utaaluma usioziungatia maadili na kuleta matokeo ya ufanyaji kazi kwa kuzingatia matakwa ya wanaofanyiwa kazi badala ya kuzingatia sheria na miongozo.

"Kuna umuhimu wa kujipanga na kufanya mabadiliko katika utendaji kazi ili kuepuka mfumo wa kufanya kazi lkwa mazoeza na kuwa na mifumo iliyojengwa ikiwa imara na itakayoisaidia wizara kutoa huduma zilizo bora zaidi"Amesema Dkt.Kijazi.