Back to top

DKT.MABULA ATETA NA MKURUGENZI WA NHC

01 July 2022
Share

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemia Mchechu Jijini Dodoma.

Mazungumzo baina ya Dkt.Mabula na Mchechu mbali na mambo mengine yalilenga kuangalia namna bora ya kuboresha Shirika la NHC sambamba kukamilisha miradi yake. 

Kwa sasa Shirika la Nyumba la Taifa linatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ile ya Ujenzi wa baadhi ya majengo ya Ofisi za Wizara katika mji wa Serikali Mtumba Dodoma, sambamba na kukamilisha miradi ya Morocco Squre na Kawe.