Back to top

Dkt.Mengi aitabiria Serengeti Boys ushindi wa goli 5 dhidi ya Nigeria

13 April 2019
Share

Mlezi wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys na kamati ya ushindi Dkt.Reginald Mengi kupitia ukurasa wake wa Twitter, amewaomba watanzania kesho Aprili 14, kujitokezan kwa wingi kuishangilia Serengeti Boys ikicheza na Nigeria, ambapo ameitabiria Serengeti Boys ushindi wa magoli matano.

Ikumbukwe Dkt.Mengi ameahidi shilingi milioni 20 kwa kila mchezaji wa timu hiyo ya Serengeti Boys endapo itashinda mechi mbili na kufuzu kucheza fainali za dunia kwa vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika nchini brazili.

Pamoja na hilo pia kamati imeahidi kutoa milioni 10 kwa chombo cha habari kitakachotoa kipaumbele zaidi katika kutangaza na kuhamasisha wananchi kuishangilia timu ya taifa ya Serengeti boys.

Wakati ikisalia siku moja sasa kabla ya kipute cha Afcon kwa vijana chini ya miaka 17 kuanza kurindima, ukarabati wa uwanja wa taifa na uwanja wa Uhuru utakaotumiwa kwa mazoezi umefikia hatua nzuri.