Back to top

Dkt.Mengi aonya Matapeli kwenye mtandao wa Facebook.

27 March 2018
Share

Mwenyekiti mtendaji wa Makampuni ya IPP Dokta. Reginald Mengi ametoa tahadhari kwa Umma kwamba hana ukurasa wa Facebook, kufuatia watu wanaotumia jina lake na picha kwenye mtandao huo.

"Ningependa kutaarifu umma kuwa sina akaunti ya Facebook".Amesema Dkt.Mengi. 

Dkt. Mengi ametoa tahadhari hiyo leo kupitia ukurasa wake wa twitter nakusema Mtu yoyote anaetumia jina au picha yake Facebook achukuliwe hatua za kisheria.