Back to top

DKT.MPANGO ATOA MAAGIZO IDOFI MAKAMBAKO

26 October 2023
Share

Makamu wa Tanzania, Dkt.Philip Mpango, ameagiza kabla ya tarehe 30 mwezi huu, apewe taarifa kwa nini baadhi ya mitambo katika kiwanda cha dawa Idofi Makambako mkoni Njombe haijafungwa kwa miaka miwili sasa.

Dkt.Mpango ametoa agizo hilo baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda hicho na kupokea kero hiyo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Makambako na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe, Bw.Deo Sanga, ambaye amesema haiwezekani mitambo ya kuchakata bidhaa nyingine isifungwe kwa mwaka wa pili sasa na kusababisha hoja kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt.Godwin Molel amesema pamoja na hoja zilizoibuliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu  wa Hesabu za Serikali na kuanza kufutwa kwa hoja hizo, lakini bado uzalishaji wa mipira ya mikono na Dawa utaendelea kufanyika Idofi na tayari waziri ameelekeza zitengwe  Shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kufunga mitambo.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Bw.Antony Mtaka, amesema mchakato wa miradi mingi ya serikali imekuwa na matatizo mengi lakini mtu binafsi akiamua kuwekeza mradi huo huo, anafanya vizuri na ndiyo sababu zinazosababisha hata kiwanda Cha Dawa Cha Idofi kuwa na hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali.