
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiambatana na mkewe mama Mbonimpaye Mpango wameshiriki ibada katika Kanisa Kuu katoliki la Bikira Maria Mshindaji Jimbo la Kigoma ambapo amewashukuru waumini, wananchi wa Kigoma pamoja na watanzania kwa ujumla kwa kumpa faraja yeye pamoja na familia kufuatia kifo cha kaka yake Askofu mstaafu wa kanisa la Anglikana Gerald Mpango.

