Back to top

DKT.NAANO AFIKA ENEO ILIPOZAMA MITUMBWI MIWILI

31 July 2023
Share

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, mkoani Mara. Dkt.Vicent Naano, amefika katika  Kijiji cha Mchigondo, ambapo watu 13, wanahofiwa kufariki dunia kwa kuzama katika Ziwa Victoria, ambapo amebainisha kuwa mitumbwi miwili iliyozama inakisiwa kuwa ilikuwa imebeba jumla watu 28, ambapo 14 wameokolewa wakiwa hai huku mmoja ambaye ni mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja akiopolewa akiwa amefariki.
.
Dkt.Naano amebainisha kuwa zoezi la uokoaji linaendelea likiongozwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji licha ya kuwa na changamoto ya hali ya hewa na tope kwenye eneo mitumbwi hiyo ilipozama.
.
Kulingana na eneo hilo lilivyo Dkt.Naano amesema kuwa wameliomba Jeshi la Polisi la Wanamaji kutoka Mkoani Mwanza, kuja kuongeza nguvu ya kutafuta miili hiyo.