Back to top

Dkt.Shein awashukia wafanyakazi wa serikalini wanaoikiuka maadili.

11 February 2020
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekit wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Ali Mohamed Shein amewaonya wafanyakazi wa Serikali ambao wanatumia nafasi zao za kazi kujitajirisha na kukiuka maadili hawataachwa na sheria itawafauata.

Dkt.Shein ametoa msimao huo alipokuwa akizumgunza baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo jipya la Mahkama Kuu Zanzibar eneo la Tunguu nje ya mji wa Zanzibar, litakalogharomu Shilingi Bilioni 14 na Milioni 300.

Amesema kuna wafanyakzi kwa makusudi wanazoretesha miradi ya maendelo kwa kusahau dhama na walizopewa.

Dkt.Shein amesisitiza azma ya seri kali yake kuona kabla hajamaliza muda wake inaboresha majengo na huduma za jamii na ameahidi ongezeko la bajeti mwaka huu.

Mapema Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe shimiwa Othman Makungu alisema uongozi wa Dkt.Shein umeweka jina kubwa nchini.