
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Jamhuri ya Indonesia, Mhe. Dkt. Puan Maharani katika Ofisi za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Bali nchini Indonesia.
Spika Tulia na Dkt Puan wamekubaliana kuenzi na kuimarisha ushirikiano baina ya mabunge ya nchi zote mbili ikiwa ni pamoja na kuongeza nguvu ya ushawishi na kuwajengea uwezo wanawake wengi zaidi kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili kuleta usawa wa kijinsia.
