Back to top

DPP amfutia kesi Lissu na wenzake, asema hana nia ya kuendelea nayo.

22 September 2021
Share

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifuta kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, Tundu Lissu na wenzake, baada ya DPP kuieleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.
.
Ilidaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifaza uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, 'Machafuko yaja Zanzibar'.
.
Kenye kesi hiyo washtakiwa hao, walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo  kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.