Back to top

Elimu zaidi inahitajika kuwalinda wafanyakazi sehemu za kazi.

20 July 2019
Share

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Christina Mndeme amesema elimu zaidi juu ya usálama katika maeneo ya kazi inahitajika kwa taasisi nchini ili kuwalinda wafanyakazi wasipate madhara wawapo katika maeneo ya kazi.

Mheshimiwa Mndeme amesema hayo mara baada ya kutembelea ofisi za wakala wa usalama na afya mahala pa kazi osha jijini Dar es salaam kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu usalama na afya kwa wafanyakazi.

Aidha amehimiza kuwa kuna uhitaji mkubwa kwa wakala huo kusogeza huduma zaidi hadi katika ngazi za wilaya jambo ambalo litasaidia kupanua zaidi wigo wao katika kusaidia wafanyakazi.