Back to top

ELON MUSK APENDEKEZA MALIPO KWENYE X.COM

19 September 2023
Share

Elon Musk Jumatatu alipendekeza kuwa mtandao wa X.COM , ambao zamani ilikuwa Twitter, hivi karibuni inaweza kuwahitaji watumiaji kulipa ada "ndogo" ili kuweza kutumia mtandao huo.

Bw Musk ameyasema hayo wakati wa matangazo ya moja kwa moja ya majadiliano na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Bw Musk alisema anaamini kuwa kutoza kwa matumizi kutapunguza watu wanaounda akaunti bandia au za roboti zinazochapisha habari za uwongo, propaganda na ulaghai.

Hakusema ni kiasi gani cha usajili wa kiwango cha chini unaweza kugharimu, au ni lini ungeanzishwa.

Majukwaa mengine ya kijamii yana changamoto na roboti, lakini Bw Musk aliwafuta kazi wafanyikazi wengi ambao wangeweza kushughulikia suala hilo.