
Mabilionea wawili wa teknolojia, Bw. Elon Musk na Mark Zuckerberg, wametangaza kuzichapa kwenye ulingo wa Vegas Octagon, uliopo Las Vegas, ambao hutumika katika mashindano Ultimate Fighting Championship (UFC).
.
Kupitia mtandao wa Twitter unaomilikiwa na Musk, Bilionea huyo alichapisha ujumbe kuwa "anajiandaa kupigana" na Mark Zuckerberg, ambapo muda mfupi baadae, Zuckerberg, ambaye ni bosi wa kampuni ya Meta, alichapisha ujumbe wa Elon Musk, huku akimjibu kuwa amtumie eneo watakalopigania, ambapo Bw. Musk, alimjibu kuwa ni Vegas Octagon.
.
Je, unadhani nani atafanikiwa kumpiga mwenzie kati ya mabilionea hao wawili?, ikiwa Elon Musk ana umri wa miaka 52 huku Mark Zuckerberg akiwa na umri wa miaka 39 tu. #via #bbc
