Back to top

EWURA kuwashushia rungu wafanyabiashara wanaokiuka masharti ya leseni

13 June 2020
Share

ARUSHA

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Bwana Godfrey Chibulunje amesema wafanyabiashara wanaokiuka sheria na masharti ya leseni Mkoani Arusha hawatavumiliwa.

Amewataka wote walioaminiwa na serikali kufanya biashara hiyo waache kukiuka masharti ya leseni zao huku akiwataka wanunuzi wa bidhaa hiyo watoe taarifa za wafanyabiashara wanaofanya vitendo hivyo, ili hatua zichukuliwe dhidi yao.

Amesema atakayekiuka sheria na masharti ya leseni za biashara atashtakiwa kwa kosa la jinai na uhujumu uchumi.