Back to top

Familia ya Mbunge wa Tarime yakubali kuchukua mwili ya ndugu yao.

01 May 2018
Share

Familia ya Mbunge wa Jimbo la Tarime vijijini Mh John Heche imekubali kupokea na kuuzika mwili wa kijana wao Suguta chacha baada ya kuridhishwa na hatua ambazo zimechukuliwa na uongozi wa serikali wilaya ya Tarime kwa kuuagiza kukamatwa na kufikishwa mahakamani askari wa Jeshi la polisi Koplo William Marwa anayetuhumiwa kumuua kijana huyo kwa kumchoma kisu.

Akizungumza baada ya kukubalina na ukoo wa familia hiyo,mmoja ya wanafamilia hiyo Mbunge wa jimbo la Tarime vijiji Mh John Heche,mbali na kulaani vikali tukio hilo la mauaji ambalo limetokea aprili 27 mwaka huu,amesema familia imekubali kuupokea mwili huo na kuuzika siku ya alhamisi wiki hii hasa baada ya mtuhumiwa huyo kufikishwa mahakamani.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa ukoo huo,wameiomba serikali kuchukua hatua sasa za kudhibiti mauaji ya raia ambao wamekuwa wakifia mikononi mwa vyombo vya dola,kwa madai kuwa kuongezeka kwa vitendo hivyo,vinaweza kujenga chuki na uhasama kati ya jamii na vyombo vya dola.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi kanda hiyo ya Tarime na Rorya Kamishina Mwandamizi wa Jeshi la polisi Henry Mwaibambe, tukio hilo la mauaji limetoea usiku wa kuamkia Aprili 27 mwaka huu,baada ya askari wa doria akiwemo na mtuhumiwa kumkamata kijana huyo akinywa pombe nje ya muda unatakiwa kisheria katika Bar moja eneo la Sirari,na wakati wa mabishano, askari huyo wa kituo cha sirari anadaiwa kumchoma kisu suguta chacha na kusababisha kifo chake.