Back to top

Familia yalala nje baada ya nyumba yao kubomolewa na Manispaa.

02 May 2021
Share

Familia ya watu saba katika mtaa wa Nyagungulu kata ya Ilemela, imeendelea kulala nje kwa zaidi ya siku 10, baada ya nyumba yao kubomolewa kwa amri ya mkuu wa idara ya mipango miji ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, kwa madai kwamba nyumba hiyo imejengwa kwenye kiwanja cha mmiliki mwingine.
.
Bi.Lucia Athanas ambaye nyumba yake imebomolewa Aprili 22 mwaka huu kwa maelekezo ya Mkuu wa Idara ya Mipango Miji Manispaa ya Ilemela Bw.Shukrani Kyando, licha ya kuwepo kwa zuio la baraza la ardhi na nyumba la wilaya ya Mwanza amesema kuwa  kwa sasa yeye na watoto wake hawana pa kuishi baada ya nyumba yao kuvunjwa.
Aidha, baadhi ya wakazi wa mtaa huo ambao wameguswa na adha anayoipata mama huyo ya kulala nje wameiomba serikali imsaidie mama huyo pamoja na watoto wake.
.
Akizungumza na ITV kwa njia ya simu Mkuu wa Idara ya Mipango Miji ya Manispaa ya Ilemela Bw.Shukrani Kyando akasema kuwa wao wanatekeleza sheria.