Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt.Doto Biteko, amewataka watumishi Serikalini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na misingi ya utoaji wa huduma, ili kuleta matokeo Chanya na sio kuwakwamisha watu wanohitaji huduma.
Dkt.Biteko ametoa agizo hilo, wakati akizindua Sera Taifa ya Biashara katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Serikalini na sekta binafsi.
Amesema katika baadhi ya ofisi kuna watu mahiri wa kuandaa maandiko lakini utekelezaji wa majukumu yao hauna uhalisia na hauendani na nyaraka walizoziandaa na hivyo nyaraka hizo kubaki kwenye makablasha.
"Tunawez a kuwa wazuri sana wa kuandika kutoa matamko na kutoa ahadi lakini hali halisi haibadiliki, Hakuna faida ya kuwa na afisa anayejipanga kumkwamisha mfanyabiashara ili tu aitwe bosi, Tunatakiwa kuwa na nyaraka inayotuunganisha wote vinginevyo sera hii itabaki kuwa kitabu cha hadithi kwenye kabati" Amesema Dkt.Biteko
Amewahimiza watumishi serikalini kuwahakikishia watu wote wanapata huduma hizo pasipo kuwekewa vikwazo suala ambalo litawajengea heshima mbele za watu wanaotafuta huduma hizo
"Uwepo wa sera ya taifa ya Biashara utasababisha mabadiliko makubwa katika nyaraka na sheria mbalimbali za nchi na hivyo sekta zote za serikali zinatakiwa kuisoma sera hii na kuisimamia" Amesema Dkt. Biteko
Katika hate nyingine, Dkt.Biteko amewataka watanzania kutumia fursa ya Sera hii kuwa nyezo ya kuimarisha nguvu za kiushindani kitaifa, kikanda na kimataifa huku akiainisha hifadhi ya mazingira na kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.