Back to top

FAO Kuboresha sekta ya uvuvi Ziwa Tanganyika

19 May 2022
Share

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kupitia mradi wake wa FISH4ACP limefanya mkutano wa pili wa Kikosi Kazi cha Taifa cha kukuza mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma kwa lengo la kujadili na kupitisha mkakati wa uboreshaji na utekelezaji wa mradi huo kama hatua ya kutatua  changamoto zinazoikabili sekta ya uvuvi kupitia mradi huo wa miaka mitano unaotekelezwa na FAO. 
.
Hayo yameelezwa na Afisa Mtaalamu Mnyororo wa Thamani wa Uvivu na Ufugaji Viumbe Maji, kutoka FAO nchini Tanzania anayesimamia mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma nchini Tanzania, Hashim Muumin amesema mradi huo unatekelezwa katika Nchi 12 za Afrika  ikiwemo  Tanzania.