Back to top

FAO KUONGEZA FEDHA ZA UNUNUZI WA CHAKULA KWA WANANCHI SOMALIA

30 November 2022
Share

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limesema limeongeza fedha za ununuzi wa chakula cha msaada kwa wananchi wa Somalia, ili kukabiliana na athari za ukame nchini humo.

Mwakilishi wa FAO nchini Somalia Bwana Etienne Peterschmitt's, amesema ukame wa sasa unaoathiri nchi hiyo ni mkali zaidi kuwahi kutokea, katika takribani miongo minne na kwamba maeneo mengi ya nchi yamekumbwa na na njaa.

Amesema utuimaji wa fedha kwa jamii za vijijini zilizo hatarini, unashughulikia mahitaji yao ya haraka na kusaidia kupunguza kuporomoka kwa maisha.

Kwa mujibu wa FAO takribani watu milioni sita na laki saba wanatarajiwa kukumbwa na uhaba wa chakula mwishoni mwa mwaka.