Back to top

FATOU BENSOUDA akamilisha ziara yake nchini Kongo.

04 May 2018
Share

Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu - ICC - Bi. FATOU BENSOUDA amekamilisha ziara yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambako amekutana na watu mbali mbali akiwemo Rais JOSEPH KABILA.

Mwendesha Mashitaka huyo alikutana Rais JOSEPH KABILA, Bazara la Maaskofu, upinzani, wanasheria na mashirika ya kiraia.

Bi.FATOU BENSOUDA alikwenda Jamhuri ya Kidemkorasi ya Kongo kufuatilia hali ya haki za binadamu.

Kwa mujibu wa Bi. FATOU BENSOUDA, serikali inajukumu la msingi la kuanzisha kesi dhidi ya wahalifu na wa naokiuka haki za binadamu nchini humo kwa lengo la kukomesha kutokujali na kurejesha hali ya haki na amani nchini.

Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Bwana FLORY KABANGE NUMBI, amemhakikishia Mwendesha Mashitaka huyo wa ICC kwamba Serikali ina uwezo wa kuchunguza kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu na kufungua mashitaki dhidi ya wahalifu hao.