Back to top

FCC yapewa siku 3 kutoa sababu za kupanda kwa bei za vinywaji

17 January 2022
Share

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mh. Ashatu Kijaji ametoa siku tatu kwa Tume ya Ushindani (FCC) kutoa sababu ya kupanda kwa bei za vinywaji baridi nchini ambapo pia ametoa siku saba kwa Tume hiyo kueleza sababu za kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi sambamba na hatua ambayo Tume hiyo imechukua kuhusiana na kupanda kwa bei hizo.