Back to top

FEDHA ZA KUMALIZIA UJENZI WA ZAHANATI ZAHITAJIKA.

19 January 2022
Share

Wananchi wa wilaya ya Nanyumbu kijiji cha Misinyasi mkoani Mtwara wameiomba serikali kutafuta fedha ili kumalizia ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho ambayo iko katika hatua za mwisho ili kuondokana na kero ya kutembea zaidi ya Kilomita tano kufuata huduma za afya katika mji wa Mangaka.

Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho ambao wamesema ujenzi wa zahanati uko katika hatua za mwisho unalazimika kusimama kutokana na fedha za kuendeleza mradi huo kumalizika.

Wanancho hao wameiomba serikali kutafuta fedha ili kumalizia sehemu iliyobaki ili kuwaondolea kero ya kutembea umbali wa zaidi ya kilomita tano kufuata huduma za afya katika mji wa Mangaka.

Kwa upande wake mtendaji wa kijiji hicho Afisiat Hamisi amekiri zahanati hiyo kutumia shilingi milioni arobaini na mbili na fedha iliyobaki kwa sasa ni shilingi milioni saba ambayo haito shi kumalizia maeneo yaliyobakia.

Akikagua ujenzi wa zahanati hiyo Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara na kamati yake ya siasa ya mkoa Yusuph Nanilla amesema Halmashauri  wanapaswa kutafuta fedha ili kumalizia sehemu iliyobaiki ili kuwaondolea adha wananchi kufuata huduma za afya mbali na maeneo yao.