Back to top

FEDHA ZISITUMIKE ZAIDI KWENYE SEMINA

07 August 2023
Share

Serikali imewataka wadau na watendaji wake kuhakikisha fedha zote zinazoingia nchini na zinazotoka serikalini kupitia ziara za nje ya nchi, za Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan zikatatue zaidi changamoto za wananchi kuliko kutumika zaidi kwenye semina na warsha.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, leo Agosti 07, 2023 wakati akizindua kampeni ya ugawaji wa vyandarua katika mikoa ya Kagera na Tabora, ikiwa ni hatua ya mapambano dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria katika mikoa hiyo.
.
"Niwaasa taasisi zote za Serikali na zisizo za Serikali, Rais wetu anapoenda kuzunguka kwenda kwenye makampuni makubwa na mashirika makubwa duniani ili kutafuta fedha, vipaumbele vyake ni kwenda kumfikia Mtanzania mnyonge kutatua changamoto katika vijiji". Amesema Dkt. Mollel.