Back to top

Freeman Mbowe ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za Ugaidi.

22 July 2021
Share

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe.Freeman Mbowe anashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kula njama na kufanya vitendo vya kigaidi ikiwemo kuua viongozi wa Serikali.

"Mbowe alikuwa anafahamu fika kuwa tuhuma zinazomkabili zilikuwa zinachunguzwa na wakati wowote angehitajika Polisi kwa hatua za kisheria mara tu uchunguzi wake utakapokamilika"-Misime.

Ameongeza kuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa kwamba, Mbowe alikamatwa kwa kuhuma za kupanga na kuandaa kongamano la Katiba mpya jijini Mwanza, jambo ambalo si kweli.