Back to top

Fuvu la binadamu wa kale kuongeza idadi wa watalii nchini.

20 July 2019
Share

Katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Prof. Adolph Mkenda amesema kuwa fuvu la binadamu wa kale zinjanthropus linalotarajiwa kuoneshwa hadharani kwa mara ya kwanza  tangu ligunduliwe mwaka 1954 katika  makumbusho ya Oldvai wiilayani Ngorongoro litatumika kuhamasisha utalii wa ndani na  nje ili kuongeza idadi ya watalii kutokana kuwa kiwakilishi muhimu katika  historia ya  binadamu duniani.
 
Akizungumza katika kongamano la maadhimisho ya miaka 60 tangu kugunduliwa kwa fuvu hilo linalojulikana kama Zinjanthropus ,katibu huyo amesema kuwa fuvu hilo ni kati ya vivutio ambavyo vikitangazwa vyema vinaweza kukuza utalii wa Tanzania.

Kamishina Mhifadhi wa  mamalaka ya hifadhi ya Ngorongoro sehemu lilipogundulika fuvu hilo Dr.Fredy Manongi amesema  tayari wameanza kufanya marekebisho ya miundombinu ya kuelekea kwenye makumbusho ya Zinjathropus..
 
Mtaalamu wa urithi wa utamaduni na mambo kale  Joshua Mwankunda , amesema  kwasasa wanajikita katika kufanya tafiti mbalimbali ili kungeza chachu katika utalii wa mambo kale.