Back to top

G7 yamkabidhi rungu Macron kukabili silaha za nyuklia Iran.

26 August 2019
Share

Kundi la G7 linaloundwa na madola saba makubwa ya viwanda duniani limemkabidhi Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa jukumu la kufikisha ujumbe na kufanya mazungumzo na Iran.

Kwa muibu wa Shirika la habari la Ufaransa limedai baada ya mazungumzo na majadiliano viongozi  hao kusini magharibi mwa Ufaransa, wamekubaliana kuwa rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron afanye mazungumzo na kufikisha ujumbe kwa Tehran kwa niaba yao.

Duru hiyo aidha imedai kwamba, kipaumbele cha madola hayo kingali ni cha kuizuia Iran isimiliki silaha za nyuklia na kuondoa hali ya wasiwasi na mivutano katika Ghuba ya Uajemi.

Kikao cha 45 cha viongozi wa nchi saba kubwa za viwanda duniani G7 ambazo ni Marekani, Uingereza, Ujerumani, Italia, Canada, Ufaransa na Japan kilianza ijumaa  katika mji wa Biarritz kusini magharibi mwa Ufaransa.