
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa familia na wananchi wa Namibia, kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo, Hage Geingob, kilichotokea leo alfajiri, Februari 04, 2024.
.
Kupitia salamu hizo za rambirambi, Rais Samia amesema Geingob, alikuwa ni Kiongozi msikivu, mtu wa watu na amekuwa miongoni mwa alama za ukombozi wa Namibia.
.
Ikumbukwe, Rais Geingob, mara ya mwisho alimpokea kwa ukarimu mkubwa Rais Samia Suluhu Hassan, mnamo Mei 07, 2023, alipokwenda kuhudhuria mkutano wa dharula wa Utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Troika).

