Back to top

GEITA: WAMTEKA MTOTO WA MIAKA 4, WATAKA MIL.4

19 January 2024
Share

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, linawashikilia watu watatu, kwa tuhuma za kumteka mtoto mwenye umri wa miaka minne, kisha kumficha, wakishinikiza kupewa Tsh. Mil. 4 ,ili waweze kumuachia.
.
Akitoa taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Bi.Safia Jongo , amesema tukio limetokea huko wilayani Mbogwe, na kwamba watekaji hao walitoa siku nne wawe wametumiwa fedha hizo, lakini Jeshi hilo limepambana na kufanikiwa kuwakamata ndani siku tatu.