Back to top

GHOROFA LAUNGUA , WATU 21 WAFARIKI GAZA

18 November 2022
Share

Habari kutoka Ukanda wa Gaza, zinaarifu kuwa, watu 21 wamekufa, baada ya moto kuzuka katika jengo lenye ghorofa tatu, katika kambi ya wakimbizi ya Jabaliya.

Tukio hilo limetajwa kuwa ni moja ya matukio mabaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni , nje ya ghasia zinazotokana na mzozo wa Israel na Palestina.

Jeshi la Ulinzi la Raia katika Ukanda wa Gaza linaloendeshwa na Hamas, limesema chanzo cha moto huo ni petroli iliyohifadhiwa kwenye jengo hilo.

Viongozi wa eneo hilo wamesema uchunguzi unaendelea.