Back to top

GOOGLE KUPUNGUZA WAFANYAKAZI 12,000

20 January 2023
Share

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Google Sundar Pichai, amewataarifu wafanyakazi wa kampuni hiyo, kuwa watapunguza takribani wafanyakazi 12,000 wa kimataifa, ambapo kupitia taarifa aliyoituma kwa wafanyakazi, kwa njia ya barua pepe alibainisha kuwa upunguzaji huo utaathiri takriban 6% ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
.
Uamuzi huo wa Google unafuata ikiwa ni siku chache tu, baada ya kampuni ya Microsoft kutangaza kupunguza wafanyakazi 10,000.