
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ametumia hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa , kutoa wito wa mshikamano na ushirikiano, ili kuunusuru "ulimwengu ulio hatarini".
Kupitia hotuba yake aliyoitoa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Guterres amesema, dunia inakabiliwa na changamoto nyingi zinazohitaji mshikamano miongoni mwa mataifa ili kuzitafutia majibu.
Amezitaja changamoto hizo kuwa ni Mabadiliko ya Tabianchi, umasikini, ukosefu mkubwa wa chakula na migawanyiko ni kitisho kwa juhudi za kufikiwa amani ya kudumu, haki za binadamu na maendeleo endelevu duniani.
#DW
