Back to top

Guterres :Kila sekunde 24, mtu anakufa kwenye ajali barabarani

22 November 2021
Share

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kila sekunde ishirini na nne  mtu mmoja anakufa kwenye ajali  ya barabarani duniani.

Amesema hayo katika Maadhimisho ya Siku ya Kukumbuka Waliopoteza  Maisha au kujeruhiwa kutokana na ajali za barabarani.

Amesema katika kuadhimisha siku hiyo ni wakati wa kutafakari juu ya vifo  vilivyosababishwa na ajali za barabarani.

Ameitaka kila nchi, kampuni na raia duniani isaidie juhudi za kitaifa na kimataifa za  kuhakikisha barabara zinakuwa salama zaidi hususani kwenye nchi za kipato cha chini na kati  ambako zaidi ya asilimia tisini ya vifo vinavyotokana na ajali barabarani hutokea.