Back to top

Gwajima apiga marufuku mikusanyiko ili kupambana na UVIKO-19.

22 July 2021
Share

Waziri wa Afya Mhe.Dkt.Dorothy Gwajima amepiga marufuku shughuli zote zinazosababisha misongamano ili kupamaba na UVICO- 19, huku akiwataka wananchi wote kujiandaa kupata huduma ya chanjo kama ambavyo Mhe.Waziri Mkuu alitoa taarifa Julai 21, 2021, kwani tayari wataalamu wa afya wamekutana kupata mafunzo kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa chanjo dhidi ya UVIKO-19 kwa hiari na bila malipo.

Kwa Mujibu wa Taarifa ya Waziri wa Afya kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa wagonjwa wa UVIKO-19 mpaka sasa nchini ni 682, ambapo amewataka wananchi kuendelea kushikamana kwenye mapambano ya kutokomeza UVIKO-19 kwa kuzingatia miongozo ya wizara hiyo ya kujikinga na kuwakinga wengine.

"Natamka kuwa kuanzia leo tarehe 22/07/2021 nimekataza shughuli zote za misongamano isiyoyalazima na ile yenye ulazima ya kutosha ichukuliwe bila kuathiri shuguli za kiuchumi na Kitaifa, Naelekeza waheshimiwa wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuwapa ushirikiano waganga wakuu wa mikoa na wakuu wa Wilaya na kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria ya afya ya Jamii Na.1 ya mwaka 2009 na kuweka utaratibu mzuri kwa wale wanaoomba vibali vya kushughuli zenye ulazima"-Amesema Gwajima.

Aidha Waziri Gwajima ametoa wito kwa viongozi wa serikali na wa sekta binafsi na taasisi zake zote kuonesha mfano kwa wananchi jinsi ya ambavyo wao wanatekeleza maagizo ya kuchukua tahadhari za kinga dhidi ya ugonjwa wa COVID-19, sambamba na wananchi kujiepusha na taarifa zozote kuhusu UVIKO-19 kupitia watoa taarifa wasio rasmi.

TAARIFA YA WIZARA YA AFYA.