Back to top

Hakimu Mfawidhi ahukumiwa miaka  3 jela au kulipa faini .

16 November 2020
Share

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya mwanzo ya Magugu mkoani Manyara Adeltus Rweyendera amehukumiwa kwenda jela kwa miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi milioni moja na nusu baada ya kupatikana na hatia kwa makosa ya kuomba rushwa na kupokea shilingi laki moja na nusu.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Holle Makungu  amesema kuwa hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Babati mkoani Manyara Isaka Kuppa ambapo mshatakiwa alitenda kosa hilo kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 2007 kifungu cha 15.