
Wizara ya Mambo ya Nje imetoa taarifa juu ya hali ya usalama ya Watanzania wanaoishi nchini Ukraine ambapo imebainisha kuwa mpaka sasa hakuna Mtanzania yoyote aliyepata madhara kufuatia hali inayoendelea nchini Ukraine huku ikiwaomba Watanzania wote wanaoishi Ukraine kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho serikali inaendelea kufuatilia usalama wao kwa kushirikiana na Mamlaka mbalimbali za nchini Ukraine.
