Back to top

Hakuna nchi inaweza kufanya uchaguzi kwa amani bila sheria-Kaijage.

28 November 2019
Share

Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage amewataka Watanzania na vyama vya siasa nchini kutambua kuwa hakuna nchi inayoweza kufanya uchaguzi kwa amani bila kufuata katiba, sheria na kanuni zinazowekwa.

Jaji Kaijage ametoa kauli hiyo jijini Mbeya wakati akizungumza na wadau wa uchaguzi ambao ni vyama vya siasa, wawakilishi wa asasi za kiraia, viongozi wa dini, machifu, vyama vya watu wenye ulemavu, vijana na wanawake,  ikiwa ni maandalizi ya kuanza zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwakani.